Naibu Rais Rigathi Gachagua amehimiza Baraza la Magavana (CoG) na mashirika ya serikali kuharakisha malipo ya bili ambazo hazijakamilika za mwaka wa kifedha wa 2022/23.

Akizungumza wakati wa mkutano uliojumuisha baraza la magavana, mashirika ya serikali na maafisa wakuu serikalini, Gachagua alisema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha inatoa fedha kwa kaunti kwa wakati unaofaa huku akishikilia kwamba serikali ilitoa fedha kwa kaunti hadi desemba mwaka jana kinyume na madai ya mwenyekiti wa kamati ya fedha katika Baraza la magavana Fernandes Baraza ambaye alisema kuwa kaunti hazijapokea fedha kutoka kwa serikali kuu tangu mwezi Novemba mwaka jana.

January 29, 2024