BY ISAYA BURUGU,7TH DEC,2023-KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini  (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini hivi leo Alhamisi.

Katika taarifa, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Machakos, Nyeri, Kirinyaga na Kajiado.Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Saika, Langata na GSU zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.Sehemu za maeneo ya Ikinu, Githiga, Munyu, Komo na Kamuthi katika kaunti ya Kiambu pia zitakosa umeme kati ya saa saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu za maeneo ya Kyumbi na Mombasa Road pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Blueline, Kakret, Kiamariga na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri pia zitakuwa bila umeme.

Sehemu za miji ya Sagana, Kagio na Kiandongu katika kaunti ya Kirinyaga pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Kajiado, sehemu za maeneo ya Namanga na Bissil zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

 

 

 

 

December 7, 2023