Katika Maisha, uwezo wa kustahimili mabadiliko kadri muda unavyosonga ni moja ya vipengee ambavyo huashiria udhibiti na ukomavu. Mila na tamaduni ya Kimaasai, ni mojawapo ya tamaduni zilizoweza kustahimili mabadiliko kwa miaka na mikaka na kusalia imara hadi katika ulimwengu wa sasa. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo yalishindwa kustahimili joto la mabadiliko, na hivyo kulazimika kudondoshwa au kubadilishwa.

Utandawazi na Maisha ya ulimwengu ya kisasa yaliyojikita katika masuala ya teknolojia, pia ni jambo ambalo limechangia kwa kudidimia kwa mil ana tamaduni, hasa jinsi mahusiano ya wanajamii yanaendelezwa. Ingawa teknolojia imerahisisha mambo, mahusiano ya moja kwa moja kati ya wanajamii yamepungua.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

March 23, 2023

Leave a Comment