Kutokana na hali ya jamii hii ya Maa kuegemea sana taasubi za kiume, kulikuwa na njia maalum ya kutangaza uwepo wa mwanume katika boma Fulani. Wanaume walitumia fimbo au mikuki hasa kwa vijana wa Morani, kuashiria uwepo wao katika boma, ili kumjulisha mwanaume mwingine kwamba kuna mwanaume mwingine kabla hajafika mlangoni.

Katika tamaduni ya kimaasai, ndoa ilikua njia kubwa ya kuunganisha koo mbalimbali, na kuhakikisha kwamba jamii inaendelea kusimama imara. Kutokana na sheria zilizowekwa ili kuzuia ndoa kati ya watu wenye damu moja, wanajamii hasa wanaume walifaidi pakubwa na kupanuka kwa uhusiano kati ya koo mbalimbali, kwani walipata hakikisho kuwa wangepokelewa eneo lolote bila tatizo.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

March 2, 2023

Leave a Comment