Shughuli ya kuiopoa miili ya wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Maasai Mara inaendelea katika mto wa Enkare Narok.

Akiongoza Shughuli hiyo ya uopozi, kamishana wa kaunti ya Narok Rueben Lotiatia amesema wawili hao walikuwa wakiuvuka mto huo ambapo mmoja wao aliteleza na kumshika mwenzake akitaka usaidizi ila wote wakatumbukia na kusombwa na maji.

Hali kadhalika Kamishna Lotiatia ametoa wito kwa wakazi wa mji wa Narok kuwa waangalifu kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa nchini.

April 25, 2024