Ntutu narok

Wakaazi wa kaunti ya Narok watanufaika na utengenezaji wa barabara, baada ya kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya miradi ya maendeleo ya Kaunti.

Gavana wa Kaunti ya Narok Patric Ntutu ameeleza kwamba awamu hii ya pili inaangazia miradi mingi ya ujenzi wa barabara, ambayo ameahidi kuwa itakamilika katika kipindi kifupi zaidi iwezekanavyo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya 15km ya Olokurto-Enesongoyo katika wadi ya Olokurto, Narok Kaskazini, Gavana ntutu alieleza kwamba miradi hii itafanikiwa kutokana na ushirikiano na wahisani wengine hasa mashirika yanayosaidia kutatua migogoro ya kifedha.

Awamu ya pili ya miradi hii inapania kuhakikisha kilomita 1,145 za barabara zinatengenezwa kote katika kaunti ya Narok, baada ya kutengewa shilingi bilioni 1.8.

May 24, 2023