Huku ulimwengu ukitarajiwa kuadhimisha siku ya usafi wa hedhi duniani hapo kesho, jamii imetakiwa kuwakumbatia kina mama na wasichana badala ya kuwatenga wanapopata hedhi zao.

Akizungumza na kituo hiki kwenye mahojiano ya kipekee, Afisa wa afya anayesimamia idara ya afya ya uzazi katika kaunti hii ya Narok Toroitich Chesang’, ameeleza kuwa wasichana wengi humu nchini hupitia unyanyapaa kutokana na hali hii.

Aidha amewahimiza kina mama na wasichana kuzingatia usafi wanapopata hedhi ili kuzuia magonjwa mbalimbali huku akiweka wazi kuwa maadhimisho hayo yataandaliwa siku ya jumatatu katika shule msingi ya Masikonde hapa mjini Narok.

Wakati hayo yakijiri takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 65 ya wanawake hawawezi wakakidhi mahitaji ya kununua sodo huku asilimia 45 hawajawahi tumia biadhaa hiyo.

Hii leo wadau wa sekta mbalimbali walikongamana katika ukumbi wa KICC kuzindua kituo cha kuhifadhia sodo ambazo zitasambazwa kwa wasichana wanaotoka kwa familia zisizojiweza kote nchini.

May 27, 2023